.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 25 Julai 2014

MAMA AJIANDALIA MAZISHI YAKE BAADA YA VIPIMO KUONYESHA KIMAKOSA ANASARATANI KALI

Mama wa watoto wawili nchini Uingereza ameelezea mateso aliyopitia kwa miaka miwili baada ya vipimo kuonyesha kimakosa anaugua saratani mbaya ambapo madaktari walimuambia ataishi kwa muda wa miaka miwili tu.

Mama huyo Denise Clark, ilibidi aandae mipango ya mazishi yake, na kuandika ujumbe wenye kuvuta hisia wa kuwaaga watoto wake wawili ambao mmoja ni mwanaume na mmoja mwanamke..

Hata hivyo Clark aliamua kwenda Hispania kupatiwa tiba mbadala ili kuongeza muda wa kuishi, na baadae baada ya kufanyiwa vipimo madaktari walibaini kile walichodhani kuwa ni saratani ni kovu lililobakia zamani wakati akitibiwa saratani katika miaka ya nyuma.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni