.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 25 Julai 2014

RAIS JK AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Ngao na Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange akitoka kuweka silaha ya jadi kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa.
Kutoka (kushoto) Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiq, wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakihudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa.
 Sehemu ya wageni waalikwa na Mabalozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo.
Askari wa Jeshi wakishiriki katika maadhimisho hayo, hapa wakiweka silaha begani.
Ni ishara ya kutoa heshima kwa Mashujaa wapiganaji.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni