.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 30 Julai 2014

MAREKANI KUJENGA KITUO CHA UONGOZI KWA VIJANA WA AFRIKA MASHARIKI

Josephine Kulea akisikiliza hotuba ya rais Barack Obama katika mkutano Jijini Washington DC.

Rais Barack Obama amesema Marekani itaanzisha kituo cha uongozi nchini Kenya ili kuwafundisha vijana wa Afrika Mashariki kumudu kushika nafasi za uongozi kwenye Biashara, Serikali pamoja na katika Asasi za kiraia.

Rais Obama amebainisha jitihada hizo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye mkutano wa Jitihada za Vijana wa Afrika Viongozi uliofanyika Jijini Washington DC na kuhudhuriwa na vijana wapatoa 450 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Mbali na Kenya Rais Obama amesema vituo vingine vya kikanda vya kuwajenga viongozi vijana wa Afrika vitafunguliwa katika nchi za Senegal, Ghana pamoja na Afrika Kusini.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni