.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 25 Julai 2014

MKE WA MICHAEL SCHUMACHER ATANGAZA KUIUZA NDEGE YA MUMEWE

Mke wa bingwa wa zamani wa mbio za magari za Langalanga Michael Schumacher, Corina ametangaza kuiuza ndege ya mumewe Schumacher ambayo alikuwa akiitumia kuisafiria katika maeneo mbalimbali dunia, kwa kiasi cha paundi milioni 12.

Kuuzwa kwa ndege hiyo siku 207 kupita tangu maisha ya Schumacher kubadilika kwa ajali ya kuteleza kwenye barafu huko Ufaransa katika Mlima Alps inaonekana kama ni ushahidi kuwa Michael hataweza tena kukabiliana na mikiki mikiki ya safari.

Schumacher, yupo katika hali ya kushindwa kutembea katika kliniki ya Lausanne huko Switzerland akiwa anafanyiwa mazoezi ya viungo na mishipa iliyopata hitilafu baada ya kuangukia kichwa wakati akiteleza kwenye barafu Desemba 29 mwaka jana.
 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni