.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 25 Julai 2014

PSPF YATOA MSAADA WA VYAKULA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA JIJINI DAR

 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi (Wa pili kulia) akimsalimia Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto Yatima (CHAKUWAMA) kilichoko Sinza jijini Dar es Salaam jana, baada ya wafanyakazi wa Mfuko huo kukabidhi misaadsa ya vyakula kwa ajili ya sikukuu ya Idd. Mfuko huo pia umekabidhi misaada kama hiyo kwa vituo vingine sita vya yatima jijini kwa ajili ya sikukuu ya Idd. Kulia ni Afisa wa fedha wa Mfuko huo, Mohammed Madenge, na kushoto ni Afisa Masoko, Magire Werema.

Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Magira Werema (Kulia) akikabidhi Mbuzi na vyakula kwa watoto wa kituo cha kulea watoto yatima cha Chakuwama Sinza jijini Dar es Salaam jana. Mfuko huo umekabidhi misada kama hiyo kwa vituo vingine sita jijini kwa ajili ya sikukuu ya Idd inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki.


Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Abdul Njaidi (Kulia) akikabidhi msaada wa vyakula ikiwemo Mbuzi kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha kulea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichoko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana. PSPF imetoa misaada kama hiyo kwa vituo sita vya yatima jijini kwa ajili ya sikukuu ya Idd.


Afisa anayeshughulikia masuala ya fedha, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mohammed Madenge, (wa kwanza kulia) akifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi (Katikati) na afisa masoko, Magira Werema, wakikabidhi msaada wa vyakula ikiwemo Mbuzi, kwa kituo cha kulea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichoko Bunju nje kidogo ya jiji jana.
PSPF, imekabidhi misaada kama hiyo kwa vituo vingine sita jijini kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki au mwanzoni mwa wiki.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni