.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 24 Julai 2014

WACHEZAJI WA MACCABI HAIFA YA ISRAEL WASHAMBULIWA UWANJANI

 Wachezaji wa timu ya Maccabi Haifa ya Israel walijikuta katika wakati mgumu baada ya kuvamiwa uwanjani na baadhi ya waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina wakati timu hiyo ilipokuwa ikicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Lille ya Ufaransa huko Austria. 

Mchezo huo ulikuwa ni sehemu ya maandalizi ya timu hizo kabla ya kuanza kwa ligi kuu katika nchi zao. 

Waandamanaji hao walivamia uwanja katika dakika ya 86 wakati tayari Lille ikiwa inaongoza kwa mabao 2-0 na kuanza kuwashambulia wachezaji wa Maccabi kwa kuwapiga, hali liliyowalazimu wachezaji hao nao kujihami kwa kupambana nao huku wengine wakikimbia kutoka uwanjani. 

Waandamanaji hao wanasadikiwa ni kutoka Uturuki ambao wanawaunga mkono Palestina katika mapigano yanyaoendelea sasa kati ya Israel na kundi la Hamas.
              Piga nikupige uwanja, kila mmoja akijaribu kujiokoa kwa kujibu mapigo
Mlinzi wa uwanjani akijitahidi kumdhibiti mmoja wa waliovamia uwanja na kuanza kuwapiga wachezaji wa Maccabi Haifa ya Israel.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni