.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 22 Julai 2014

WATU WANANE WAKAMATWA KWA KUTUPA MABAKI YA MIILI YA BINADAMU JIJINI DAR

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu wanane kwa kuhusika na tukio la kutupa mabaki ya miili ya binadamu katika msitu mdogo uliopo eneo la Mpiji, Kata ya Mbweni, Wilaya ya Kinondoni.

Akiongea leo Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova, amesema miongoni mwa watu waliokamatwa wamo pia madaktari wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU), ambapo miili hiyo ilikuwa imehifadhiwa kwa ajili ya mafunzo.

Kamanda Kova amesema kuwa jeshi la polisi limeunda jopo la watu saba la maafisa wa upelelezi linaloongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jafari Mohamed ili kubaini sababu zilizopelekea Chuo cha IMTU kutupa viungo hivyo vya Binadamu maeneo hayo.

Aidha, Kamanda Kova amesema jeshi la polisi pia litawahusisha Mkemia Mkuu wa Serikali na Mwanasheria Mkuu ili kubaini miili hiyo ni ya kina nani ilipatikana vipi na kwa kibali gani ikiwa ni pamoja na kufahamu hatua za kisheria zitatumika kuwaadhibu wahusika.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni