.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 31 Julai 2014

WAZIRI MKUU MH PINDA MGENI RASMI MTWARA FESTIVAL 2014

Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akiwa katika picha na Bw. Anic Kashasha, Mwenyekiti Mtendaji wa TACIN alipomtembelea nyumbani kwake Oyserbay, Dar es Salaam, kumpa taarifa ya maendeleo ya maandalizi ya Mtwara Festival, itakayofanyika tarehe 16 - 17 Agosti, 2014 katika viwanja vya Chuo Cha Ualimu Mtwara(TTC).

Mh. Mizengo Pinda, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi wa Mtwara Festival, ambao ni mpango mkakati wa mawasiliano wa kuhamasisha wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi, kizitambua fursa shirikishi zinazosisimuliwa na uchumi wa gesi asilia.

Kauli mbiu ya Mtwara Festival ni "FURSA ZIMEFUNGUKA, TUZITAMBUE, TUJIANDAE, TUZICHANGAMKIE". Akizungumza mara baada ya kukutana na Waziri Mkuu, Bw. Kashasha alisema mpango huo wa elimu kwa umma, utachangia kwa kiasi kikubwa kutengeneza ajira na kipato kwa wananchi wa mikoa hiyo na hivyo kubadilisha hali za maisha ya wananchi hao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni