Timu ya Arsenal ipo tayari kuchuana
na Manchester United kumtwaa beki wa katika Mjerumani, Mats Hummels.
Hadi sasa Manchester United
wameshindwa kukubaliana dau la paundi milioni 25 lililowekwa na timu
yake ya Borussia Dortmund.
Arsenal, inaweza ikakamilisha kutoa
kitita hicho na kumtwaa Hummels, baada ya kupata fedha walizomuuza
Thomas Vermaelen kwenda Barcelona siku ya jumamosi.
Manchester United pia inatarajia
kunasa saini ya Juan Cuadrado mwishoni mwa wikii hii.
Juan Cuadrado (kushoto) akichuana na Marcelo


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni