Marekani imeendelea kufanya
mashambulizi ya anga pamoja na kudondosha misaada nchini Irak, wakati
Rais Barack Obama akiapa kusaidia kuwaokoa maelfu ya raia
waliozingirwa na wapiganaji wa kundi la Taifa la Kiislam (IS) kwenye
mlima Sinjar.
Rais Obama ametoa ratiba ya
operesheni ya jeshi la Marekani nchini Irak, tangu kundi la mwisho la
Marekani kuondoka nchini humo miaka mitatu iliyopita, na kuitaka
serikali ya Irak kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na kuwadhibiti
wapiganaji wa vita vya jihadi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni