Askari huyo feki wa Usalama Barabarani ambae Jina lake halikufahamika haraka akiwa chini ya Ulinzi mkali wa Askari Polisi mara baada ya kukamatwa kwa kujifanya ni askari wa usalama barabarani huku akifahamu kuwa ni kosa kisheria.
Inasemekana Mtuhumiwa aliwahi kuwa askari wa Usalama barabarani ambapo kituo chake cha Kazi kilikuwa Mkoa wa Pwani, na ni mmoja kati ya askari waliofukuzwa kazi kwa kuenda kinyume na taratibu na sheria za Jeshi la Polisi Tanzania.
Picha Kwa Hisani ya Mdau

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni