Mholanzi, Louis van Gaal uhenda akawa na msimu mzuri katika ligi kuu ya Uingereza akiwa na timu ya Manchester United, baada ya kuendelea kufanya vyema katika michezo yake yote ya kujiandaa na msimu mpya wa Barclays Premier League inayotarajia kuanza kutimua vumbi August 16'2014.
Ikicheza mbele ya watazamaji 109,318 katika uwanja wa Michigan nchini Marekani, Manchester United iliichapa Real Madrid mabao 3-1 na kuwafanya United kuendelea kuimarika kwa kasi toka kufika kikosini hapo Van Gaal.
Mabao ya Manchester United yaliwekwa kimiani na Ashley Young ambaye alipachika mabao mawili katika dakika za 20 na 37 kisha Javier Hernandez akafunga bao la tatu katika dakika ya 80.
Bao la Madrid lilifungwa katika dakika ya 27 , mfungaji akiwa na mshambuliaji Gareth Bale kwa mkwaju wa penati.
Kwa matokeo hayo, sasa United itakutana na Liverpool katika fainali ya michuano hiyo ya International Champions kesho jumatatu.
Mashabiki wakiwa wamefurika katika uwanja wa Michigan, ambao idadi yao ilikuwa 109,318.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni