Didier Drogba ameichezea kwa mara ya
kwanza Chelsea hapo jana hata hivyo akajikuta akikaribishwa na kipigo
cha mabao 3-0 kutoka kwa Werder Bremen ya Ujerumani.
Kipa Thibaut Courtois naye
aliichezea Chelsea kwa mara ya kwanza baada ya kucheza kwa mkopo
miaka 3 akiwa na Atletico Madrid.
Chelsea ilizamishwa kwa mabao ya
penati ya Eljero Elia na Felix Kroos pamoja na bao la kichwa la
Ludovic Obraniak na kutosha kabisa kuipa ushindi timu hiyo ya Ligi ya
Bundesliga.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni