
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa tatu kushoto) akisaini hati za makubaliano ya mkopo wa shs bilioni 100 na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohamed Enterprises Ltd (METL), Mohamed Dewji kwa ajili ya kampuni dada ya METL ya Star Oils inayoshughulika na biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni baadhi ya watendaji wakuu wa NBC, METL na Star Oils.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji wakionyesha mikataba muda mfupi baada ya kusaini hati za makubaliano ya mkopo wa shs bilioni 100 kwa ajili ya kampuni dada ya METL ya Star Oils inayoshughulika na biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bi Mizinga Melu akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya kuipatia kampuni ya Star Oils mkopo wa takribani sh bilioni 100 ili kuongeza ufanisi katika kampuni hiyo ya uagizaji na usambazaji wa mafuta nchini.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni