.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 4 Agosti 2014

ISRAELI YATANGAZA KUSITISHA MAPIGANO LEO HUKO GAZA KWA MUDA WA SAA SABA

Nchi ya Israeli imetangaza kusitisha mapigano kwa saa saba kwa ajili ya utoaji huduma za misaada ya kibinadamu huko Gaza kuanzia leo asubuhi.

Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Israeli amesema usitishaji mapigano hayo hautahusisha mji wa Rafah, na kuongeza kuwa wanajeshi wake watajibu mapigo iwapo watashambuliwa.

Mapema Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alielezea kitendo cha Israeli kushambulia shule ya Umoja wa Mataifa huko Gaza kama si chauadilifu na ni kitendo cha uhalifu.

Shambulio katika shule hiyo limeelezwa na Mamlaka za Palestina kuwa limesababisha vifo vya watu 10, hapo jana.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni