.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 23 Agosti 2014

EXTRA BONGO KUISINDIKIZA MASAI SAFARI BAND



Na Mwandishi Wetu

BENDI ya Masai Safari ya jijini Dar es salaam inatarajia kuzindua albam yake ya kwanza kabisa watakayozindua siku ya August 30 katika ukumbi wa Launch Time ya jijini.


Akizungumzia uzinduzi wa albam hiyo, rais wa bendi hiyo Fransic Mwaisela amesema kwamba siku hiyo watasindikizwa na bendi mbalimbali wakiongozwa na bendi ya Extra bongo inayoongozwa na Ali Choki.

Alizitaja nyimbo zilizomo katika albam hiyo ni sita itakayozinduliwa siku hiyo ikiwa nyimbo ambayo imebeba albam ni " akuna kama baba" ya pili ni njia panda,mikono ni kazi,ndoa ni mpango wa mungu,usiwasikilize wambeya,kilio changu nyimbo hizo ndio zitakazokuwa katika albam hiyo itakayo zinduliwa mwishoni mwa mwezi huu.

Aliongeza kwa kutaja wasanii wengine watakaokuwepo siku hiyo ni Omari Tego,Maua Tego pamoja na wasanii mbalimbali wa bongo fleva watakaosindikiza uzinduzi huo.

Bendi hiyo kwa sasa ipo kwenye mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kutoa burudani kabambe siku ya uzinduzi wa albam ya bendi hiyo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni