.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 23 Agosti 2014

RONALDO, BALE, RODRIGUEZ WASHINDWA KUISAIDIA REAL MADRID MBELE YA ATLETICO WALIOTWAA UBINGWA WA SUPER CUP

 Atletico Madrid ndio mabingwa wa kombe la Super Cup 2014 baada ya kuifunga Real Madrid bao 1-0 katika mchezo wa marudiano uliochezwa usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Vicente Calderon. 

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Santiago Bernabeu, timu hizo zilifungana bao 1-1, hivyo Atletico Madrid kwa ushindi huo wa jana wametwaa kombe hilo kwa tofauti ya mabao 2-1. 

Real Madrid ikiwa na nyota wake wote akiwemo Cristiano Ronaldo, Gareth Balle na James Rodriguez walishindwa kabisa kufurukuta mbele ya vijana wa kocha asiyetulia hata mara moja katika eneo lake Diego Simeone. 

Bao hilo muhimu la Atletico Madrid lilifungwa mapema kabisa katika dakika ya pili ya mchezo na mchezaji Mario Mandzukic.
 Mshambuliaji hatari wa Atletico Madrid, Mario Mandzukic akiwa amelinyanyua juu kombe la Super Cup
                       Raha ya ubingwa! Kikosi cha Atletico Madrid wakiwa na kombe lao
Mario Mandzukic akikimbia kwa furaha mara baada ya kufunga bao katika dakika ya pili ya kipindi cha kwanza na kuifanya Atletico Madrid kutwaa kombe la Super Cup.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni