.jpg)
Msanii nguli wa muziki wa hip hop professor J (kulia) akimkaribisha jukwaani msanii mwenzake wa hip hop na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu wakati wa tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 linalodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Na mwandishi wetu
Tamasha la Kili Music Tour linalodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager limeacha gumzo kubwa jiji la Mbeya baada ya kufanyika kwa show ya aina yake iliyowaleta pamoja wasanii wakubwa na kuwavuta maelfu ya wakazi wa Mbeya.
Onyesho hilo la aina yake, lilifanyika katika Ukumbi wa New City Pub ambapo wasanii 10 ndio walitoa burudani kwa masaa sita mfululizo ambapo onesho lilianza saa mbili usiku na kuisha saa nane.
Wasanii waliopanda katika jukwaa la tamasha hilo mkoani Mbeya walikuwa ni pamoja na Chibwa, Rich Mavoko, MwanaFA, AY, Profesa Jay, Izzo B, Joh Makini, Nikki wa Pili, G Nako na Shilole na walishangiliwa kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Moja kati ya matukio mazuri na ya kusisimua yaliyotokea katika tamasha hilo ni wakati Profesa Jay alipokuwa jukwaani, kumshawishi Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ambaye pia ni msanii wa Hip Hop kupanda jukwaani na kuiwakilisha Hip Hop kwa wananchi wake.

Sugu alipanda jukwaani na aliongea machache kuhusiana na Tamasha la Kili na kuhamasisha amani miongoni mwa mashabiki wa muziki ambao walionekana kuwa wengi kuliko kiwango kilichotegemea na kuvunja rekodi ya uwanja huo wa Mbeya.
Izzo B, ambaye alitajwa kama mwenyeji wa tamasha hilo mkoani Mbeya alipanda jukwaani akiwa amevalia ki`manamba', (..shati jeupe na kaptula na viatu vyeusi na soksi ndefu nyeupe) kinyume na anavyovaa siku zote anapokuwa katika matamasha hali iliyochangia kuleta msisimko mwingine.
Pamoja na burudani kubwa pia kulikuwa na nyamachoma ya kutosha ambayo ilienda sambamba na Bia za Kilimanjaro Premium Lager kwa wenye umri zaidi ya miaka 18.
Mbeya ndio mkoa wa kwanza katika awamu ya pili ya ziara hii ya wasanii ambayo tayari imeshapita katika mikoa mitano katika awamu ya kwanza ikiwemo Kilimanjaro, Mwanza, Kahama, Ruvuma na Iringa.
Tamasha hili linaratibiwa na makampuni ya East Africa Television, East Africa Radio, Executive Solutions, Aggrey and Clifford, Integrated Communications na Aim Group.

Wasanii wote wameipongeza Kilimanjaro Premium Lager kwa maandalizi mazuri na pia kuthamini kazi ya wasanii kwa kuwalipa vizuri na pia kuwawezesha wapeleke kazi zao kwa wananchi.
Jumamosi hii ya tarehe 16 Agosti, tamasha hilo linaloonekana kuwa na mvuto wa aina yake linatarajiwa kuelekea Dodoma ambako wasanii zaidi ya 10 watashiriki.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni