Makubaliano mapya ya kusitisha
mapigano kwa muda wa siku tatu baina ya Israel na kundi la Hamas huko
Gaza yanaanza utekelezaji wake leo.
Makubaliano hayo yalioanzia saa sita
usiku wa jumapili, yamekuja baada ya siku kadhaa za majadiliano ya
upatanishi.
Iwapo makubaliano hayo yataheshimiwa
Israel itatuma ujumbe wake Jijini Cairo hii leo kwa ajili ya
kujadiliana kusitisha kabisa mapigano hayo yaliyosababisha vifo vya
watu 2,000 tangu yaanze Julai 8.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni