.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 4 Agosti 2014

MASHABIKI WA HARAMBEE STARS WATAKA KUMALIZA HASIRA ZAO KWA VICTOR WANYAMA

Kapteni wa Harambee Stars Victor Wanyama ameokolewa kutoka kwa kundi la mashabiki wenye hasira Jijini Nairobi baada ya Harambee Stars kutolewa nje ya michuano ya kuwania kufuzu kutinga michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika na timu ndogo ya Lesotho.

Kiungo huyo wa timu ya Southampton ilibidi atolewe uwanjani na kukimbizwa sehemu salama na polisi wa Kenya, baada ya Harambee Stars kudhibitiwa na kutoka sare tasa, na kuifanya Lesotho kusonga mbele kwa ushindi wa awali wa bao 1 bila walioupata nyumbani.

Mara baada ya matokeo hayo Kenya ilimtimua kazi kocha Adel Amrouche, raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria, kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Kenya.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni