.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 4 Agosti 2014

MTWARA FESTIVAL KUFANYIKA VIWANJA VYA CHUO CHA UALIMU MJINI MTWARA AUG 16-17'2014

Tanzania Creative Industries Network (TACIN) kwa kushirikiana na TPDC wanakuletea Tamasha kubwa la Mtwara Festival katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Mjini Mtwara kuanzia 16 hadi 17  mwezi huu wa nane mwaka 2014.

Mtwara Festival ni jukwaa endelevu la kuwaleta pamoja wana Mtwara na Lindi wakifurahia tamaduni zao, huku wakihamasihwa na kupata taarifa juu ya fursa mbali mbali za ajira na kipato zinazotokana na uwekezaji unaoongezeka kwa kasi kubwa.

Kauli Mbiu ni “Fursa zimefunguka, Tuzitambue, Tujiandae na Tuzichangamkie “.

Mtwara Festival 2014 itakuwa ni mchanganyiko wa burudani na utalii, na pia  itakuwa na fursa kwa wafanyabiashara pamoja na sekta binafsi kutangaza biashara na huduma zao.

Ili kushiriki tamasha hili la aina yake, wasilisha maombi yako sasa kupitia namba za simu, 0754 280 491 au 0784 280 491.

Mtwara Festival 2014, Imedhaminiwa na TPDC, PSPF, Tanzania Distilleries Ltd, Air Tanzania na PPF.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni