Afisa Mshiriki wa Maonesho ya
Wakulima na Wafugaji katika Banda la Jeshi la Magereza, Mrakibu
Msaidizi wa Magereza, Yunge Saganda (kushoto) akitoa maelezo ya
kitalaam kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe. Regina Chonjo(kulia)
namna viatu vya Ngozi vinavyotengenezwa na Jeshi hilo katika Kiwanda
chake cha Gereza Karanga, Moshi Mkoani Kilimanjaro. Jeshi la Magereza
ni Miongoni mwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinavyoshiriki
kikamilifu katika Maonesho hayo ya Kitaifa Mkoani Lindi.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe.
Regina Chonjo (wa pili kushoto) akiangalia Mbegu ya Ufuta
inayozalishwa na Jeshi la Magereza kupitia miradi mbalimbali ya
Kilimo katika Magereza ya Kilimo hapa Nchini(wa kwanza kulia) ni Mkuu
wa Magereza Mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza,
Tusekile Mwaisabila.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe.
Regina Chonjo akikagua Bustani ya Shamba Darasa iliyopo katika Banda
la Jeshi la Magereza katika Viwanja vya Maonesho vya Ngongo, Mkoani
Lindi. Bustani hiyo iliyostawishwa kwa kufuata Kanuni za Kilimo Bora
na Biashara inatumika kutoa elimu kwa Wakulima wanapotembelea Banda
hilo katika Maonesho haya ya Kimataifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe.
Abdallah Ulega(kulia) akisalimiana na Mkuu wa Magereza Mkoani Lindi
alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza ili kujionea shughuli
mbalimbali za Kilimo na Ufugaji zinazofanywa na Jeshi hilo katika
Maonesho hayo ya Nane Nane. (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la
Magereza).




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni