.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 8 Agosti 2014

MTU MMOJA AHISIWA KUUGUA UGONJWA HATARI WA EBOLA

Maafisa wa Wizara ya Afya ya wa Uganda wamemuweka mtu mmoja anayeshukiwa kuugua ugonjwa wa Ebola katika chumba cha pekee yake katika hospitali ya Daraja B ya Entebbe.

Mkurugenzi Mkuu Huduma za Afya katika wizara hiyo, Dk. Jane Aceng, amesema mtu huyo ambaye ni mtumishi wa afya alibainika kuwa na ugonjwa huo alipofanyiwa vipimo katika uwanja wa Entebbe wakati alipowasili.

Mgonjwa huyo alikuwa anafanya kazi na shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, Sudani Kusini, ambapo aliletwa Kampala kwa ajili ya matibabu ya homa ya inni, lakini imebainika kuwa huenda ni Ebola.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni