Nyota wa Mpira
wa Kikapu wa Indiana Pacers Paul George amepoteza matumaini ya
kucheza Michuano ya Kombe la Dunia, baada ya kuvunjika mguu wakati wa
mazoezi ya timu ya taifa ya Marekani huko Las Vegas.
George ambaye
ameshakua mchezaji bora mara mbili wa Ligi Kuu ya Kikapu ya NBA,
alikuwa akifanya mazoezi na kikosi mchanganyiko cha Marekani,
alipoumia vibaya na kuvunjika mguu wakati akitua kwa nyuma.
Baada ya tukio
hilo George ilibidi abebwe kwa machela na kutolewa uwanjani huku
wachezaji wenzake wa Marekani wakimuangalia kwa mshtuko kufuatia
tukio hilo.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni