.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 3 Agosti 2014

TETEMEKO LA ARDHI LAUWA WATU 150 NCHINI CHINA

Watu wapatao 150 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 6.1 kulikumba eneo la kusini magharibi mwa China hii leo.

Wataalamu wa Masula ya Miamba wa Marekani wamesema tetemeko hilo limelikumba eneo la kilomita 11 kaskazini magharibi mwa mkoa wa Wenping Yuannan majira ya saa kumi na nusu saa za huko.

Mmoja wa maafisa wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la china la Xinhua kuwa nyumba nyingi zimeporomoka.

Shirika la Utangazaji la taifa la China la CCTV, limesema kuwa tetemeko hilo ni kubwa kuwahi kutokea katika mkoa huo tangu miaka 14 kupita.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni