Rais Barack Obama ameamuru
kutekelezwa kwa mashambulizia ya anga dhidi ya wapiganaji wa Kiislam
wa Kaskazini mwa Irak, hata hivyo amesema hatorudisha majeshi ya
Marekani nchini humo.
Amesema wapiganaji wa Dola ya
Kiislam (IS), watalengwa katika mashambulizi hayo ili kudhiditi
vitendo vya mauaji vinavyofanywa dhidi ya watu wa madhehebu mengine
madogo, na kuhatarisha masilahi ya Marekani.
Mashambulizi hayo ya anga
hayajaanza, hata hivyo Marekani imekuwa ikidondosha misaada ya
kibinadamu kwa njia ya ndege kutokana na tishio la wapiganaji hao.
IS wametwaa mji mkubwa wanaoishi
Wakristo nchini Irak wa Qaraqosh, na kuwafanya wakazi wake kuukimbia.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni