.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 8 Agosti 2014

WAKILI WA OSCAR PISTORIUS ADAI UPANDE WA UTETEZI ULIVURUGA USHAHIDI MUHIMU

Kesi ya mauaji ya mwanamitindo Reeva Steenkamp inayomkabili mwanariadha mlemavu,Oscar Pistorius wa Afrika Kusini, imeendelea leo ambapo upande wa utetezi umewasilisha utetezi wao wa mwisho.

Wakili Barry Roux na timu yake ya utetezi, katika maelezo yao wamewalaumu polisi kwa kuvuruga ushahidi muhimu katika eneo la tukio na hivyo kufanya ushahidi uliotokana na eneo la tukio kuwa si halali.

Upande huu wa utetezi umetumia muda wake wa kukamilisha hoja zao katika kesi hiyyo kwa kuuhumu upande wa mashtaka kwa kesi hii kwa makosa ya udanganyifu na kuharibu ushahidi.

Wakili Barry Roux amesema mwanariadha huyo mlemavu aliyekatwa miguu yake miwili, anapaswa kukabiliwa na shtaka la kuua bila ya kukusudia, na si kesi ya mauaji ya mpenzi wakeReeva Steenkamp.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni