Watu wapatao 10
wameuwawa katika shambulio la anga lililofanywa Israeli kwenye shule
ya Umoja wa Mataifa, inayotumika kuhifadhi Wapalestina waliokimbia
mapigano huko Gaza.
Shambulio hilo
limelenga mlango wa kuingilia shule hiyo huko Rafah, ambapo maelfu ya
Wapalestina wamepatiwa hifadhi.
Jeshi la Israeli
halijatoa tamko lolote, licha ya kuanzisha mashambulizi mapya huko
Gaza, yaliyopelekea vifo vya watu 30 hii leo, huku nao wapiganaji wa
Hamas wakiendelea kurusha makombora ya roketi Israeli.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni