Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, ACP Suzan Kaganda akiwaonyesha waandishi wa habari chesesi namba iliyoharibiwa ya moja kati ya magari matano yaliyokamatwa na jeshi hilo
Sare za jeshi la wananchi, milipuko aina ya Magnam Blaster, Bunduki na Bastola zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoani Tabora.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 04/08/2014.
Ndugu waandishi wa habari, Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora linaendelea na operesheni ya kupamabana na uhalifu na wahalifu katika wilaya zote za mkoa wa tabora. Katika operesheni zianazoendelea tumefanikiwa kama ifuatavyo:-
KUPATIKANA KWA SILAHA AINA YA:-
1. GOBORE- 01
2. PISTOL - 02 ZILIZOTENGENEZWA KIENYEJI.
3. SMG - 01 IKIWA NA MAGAZINE 2 TUPU
katika wilaya ya Urambo imekamatwa silaha aina ya SMG yenye No BIPNUB 7328 ikiwa na magazine mbili tupu, Kupatikana kwa silaha hiyo kumetokana na msako mkali ambao ulikuwa unafanywa na jeshi la Polisi na hivyo watuhumiwa wasiojulikana walitelekeza bunduki hiyo iliyokuwa imefichwa ndani ya shimo na juu yake kumepangwa tofali, aidha huko Usoke kufuatia taarifa za wananchi imekamatwa silaha aina ya gobore moja lililokuwa likimilikiwa isivyo halalali. Aidha katika wilaya ya Uyui eneo la kigwa zimekamatwa silaha mbili aina ya pistol zilizotengenezwa kienyeji. Watuhumiwa waliokamatwa na silaha hizo ni:-
1. SELEMANI S/O HARUNA @LETA 40yrs Mnyamwezi, mkazi wa Kigwa.
2. RAJABU S/O IDDI 28YRS, Msukuma mkazi wa kigwa
3. HAMISI S/O JUMA, 45yrs, Muha, mkazi wa Kangeme
Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
KUPATIKANA NA MILIPUKO: -
Huko wilaya ya Nzega amekamatwa AMONI s/o BITEGEKO, 22yrs, Mhaya mkazi wa Isunga- Nzega akiwa na vifaa vya milipuko aina ya MAGNAM BLASTERM.50, DENOTING CONDUCTOR MTR. 15 nyumbani kwake. Baada ya kuhojiwa mtuhumiwa ameshindwa kutoa ufafanuzi juu ya umiliki wa milipuko hiyo. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
KUPATIKANA NA MAGARI MATANO YADHANIWAYO KUWA YA WIZI:
katika hatua nyingine kufuatia wizi wa magari ulifanyika msako na yalikamatwa magari matano yenye namba za usajili: T.924 AXB Toyota Harrier, T.734 CFT Toyota IST, T546 APD Toyota Carina, T. 588 AGB Toyota Land Cruiser (PRADO), T.376 ADA Toyota Carina – TI. Wamiliki wa magari hayo walipohojiwa walimtaja ATHUMANI S/O HAMISI JUMANNE, 32YRS, M/Mwezi, mfanyabiashara, mkazi wa Mwinyi manispaa ya Tabora ndiye aliyewauzia magari hayo ambayo na ye ameshindwa kutoa uthibitisho halali wa jinsi alivyoyapata magari hayo. Uchunguzi wa awali unaonesha chasisi za magari hayo zimeharibiwa. Mfanyabiashara huyo anashikiliwa na jeshi la Polisi na upelelezi bado unaendelea ili kubaini mtandao wa wizi wa magari.
KUPATIKANA NA SARE ZA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA: -
katika Manispaa ya Tabora wamekamatwa watuhumiwa watatu (03) kwa kosa la kukutwa na sare za JWTZ ambao ni:-
1. ISACK S/O ALBANO@MLOLI, 44yrs, Mfipa, mkazi wa Isandura-Magu Mwanza.
2. WILIAM S/O JAMES@ KAPUFI, 34yrs, Mfipa,. mkazi wa Msange Tabora.
3. MSAFIRI S/O JUMANNE@ MHALILI, 25yrs, Mfipa, mkazi wa Msange Tabora.
Baada ya mahojiano watuhumiwa wamekiri kuwatishia wananchi na kujipatia kipato kutokana na sare hizo. Aidha watuhumiwa hao wamekiri kujihusiha na matukio ya uhalifu ikiwemo wa kutumia silaha hapa manispaa na wilaya jirani. watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora linazidi kutoa rai kwa wanachi kuzidi kushirikiana nasi katika kupambana na uhalifu na wahalifu, na pia operesheni hii ni endelevu.
Imetolewa na:-
Suzan S. Kaganda –ACP.
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA TABORA.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni