.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 31 Agosti 2014

TAMASHA LA KILI MUSIC TOUR LAFANYA KWELI TANGA


Wasanii wa kundi la Weusi linaloundwa na Joh Makini, Nikki wa 2, G-Nako toka kaskazini mwa Tanzania, jijini Arusha wakitoa burudani katika Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika jana Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Rich Mavoko akiwapagawisha mashabiki wa mji wa Tanga waliohudhuria katika Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika jana Uwanja wa Mkwakwani. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

Wakazi wa jiji la Tanga na vitongoji vyake wakiwa katika Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa Mkwakwani. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki na Afrika kwa Ujumla, Bi. Khadija Omary Kopa akitoa burudani ya Kikwetu Kwetu sambamba na mmoja wa wacheza shoo wake katika Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Ben Pol akitoa burudani katika Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika jana Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ommy Dimpoz akiwapagawisha mashabiki wa wakazi wa jiji la Tanga katika Tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2014 lililofanyika jana Uwanja wa Mkwakwani. Tamasha hili limedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni