Wapiganaji wa Kikurd wa kikosi cha
peshmerga wametumia matrekta, malori pamoja na punda kuwaondoa katika
eneo hilo, baada ya kukosa misaada kutokana na vikosi vya Marekani
kuendelea kuwashambulia kwa anga wapiganaji wa Kiislam.
Baadhi ya watu wa kundi hilo la
kabila ndogo la Yazidi, walilazimika kuondolewa eneo hilo kwa miguu,
wakipitia kwenye jangwa, ambapo inaaminika karibu watu 5,000
walipelekwa mahala salama na wapiganaji wa Kikurd. Bado kuna maelfu
yao wapo katika maeneo hatari kwenye mlima Sinjar.
Mama akiwa juu ya punda akiondolewa eneo hatari na wapiganaji Wakikurd



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni