Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa
Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP) Godfrey Mulisa akisoma
risala ya ufunguzi wa warsha hiyo kwa niaba ya Philippe Poinsot
inayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya Waziri Mkuu mjini
Dodoma.
Mwenyekiti wa mtandao wa vyombo vya
habari vya kijamii Tanzania (COMNETA) ambaye pia ni Mkurugenzi wa
Redio ya Jamii FADECO wilayani Karagwe, Bw.Joseph Sekiku akieleza
kwa ufupi maendeleo ya COMNETA wakati wa sherehe za ufunguzi za
mkutano wa tano wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii nchini
(COMNETA) unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Waziri
Mkuu mjini Dodoma.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), Jaji John J. Mkwawa, akitoa mada kwa wadau wa
utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia amani
nchini (DEP) katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu ujao,
unaofadhiliwa na Shirika La Kimataifa la Maendeleo (UNDP) ) katika
warsha ya siku nne inayoendelea mjiji Dodoma. Kutoka kulia ni Afisa
Habari na Mahusiano Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Bi. Salha Ali, Bi.
Margaret Rugambwa mtalaam wa masuala ya jinsia na jamii kutoka UN
Women na Mgeni rasmi Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la
Kimataifa la Maendeleo (UNDP) Godfrey Mulisa ambaye pia ni Mtaalam wa
masuala ya utawala bora kutoka UNDP.Na Mwandishi wetu
Uchaguzi huru na wa haki utafanikiwa
iwapo wananchi watapewa elimu sahihi ya uraia na upigaji kura
itakayohamasisha wapiga kura kufanya maamuzi sahihi wakati wa
uchaguzi.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji John Mkwawa kwenye washa ya siku nne
ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa uchaguzi unaolenga kuboresha
demokrasia na amani nchini kuelekea uchaguzi mkuu ujao .
Kamishina alisema elimu ya uraia ni
muhimu kwa wananchi ili kuwahamasisha ushiriki wao katika demokrasia
na kwamba haipaswi kuwa na utashi wa kisiasa au upendeleo kwa chama
chochote cha siasa.
Akitoa mada katika warsha hiyo
inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
maendeleo (UNDP) Jaji Mkwawa alisema katika kutoa elimu hiyo
wanahabari hawana budi pia kuzingatia miongozo iliyowekwa ya
kutofungamana upande wowote kisiasa na kutoa habari kwa usahihi
kuhakikisha kwamba makundi yote yanapewa fursa na haki sawa.
Amependekeza pia umuhimu wa kuielewa
jamii inayolengwa wakati wa kutayarisha vipindi vya elimu ya uraia na
utekelezaji ili taarifa zinazotolewa kwao zikidhi matakwa ya sehemu
hiyo.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji John Mkwawa ametoa mfano wa kuilewa jamii kuwa ni
pamoja na kufahamu sababu zinazowafanya wananchi wasijitokeze kwa
wingi katika upigaji kura iwapo kunasababishwa na ukosefu wa taarifa
muhimu na sahihi, kukosa motisha ya kupiga kura, utashi na kutokuwepo
kwa ushindani katika kugombea.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni