Bibi Maryam Khamis (Wapili kulia)
Mtaalam wa uchumi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Zanzibar
akizungumza katika kikao hicho.
Pichani ni baadhi ya viongozi
waliohudhuria Kikao hicho. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Dkt. Adelhelm Meru.
Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho, Bw.
Aunyisa Meena kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara akichangia mada.
Na Saidi Mkabakuli
Wapanga mipango nchini wameaswa
kuzingatia weledi wakati wa kuandaa maandiko ya miradi
yanayowasilishwa kwa wafadhili ili kuongeza ushindani dhidi ya nchi
nyingine wakati wa uwasilishaji wa maombi ya kupatiwa ufadhili wa
miradi ya maendeleo.
Wito huo umetolewa na Kaimu Katibu
Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri
wakati alipofanya mazungumzo na viongozi waandamizi kutoka wizara za
viwanda na biashara, fedha, uchukuzi, nishati na madini pamoja na
viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Zanzibar.
Bibi Mwanri alisema kuwa kuna
ushindani mkubwa kwa nchi zinazoomba ufadhili wa miradi ya maendeleo
hivyo uandishi wa maandiko yenye kuzingatia weledi na viwango vya
kimataifa ni msingi katika kuongeza ushindani na kuweza kuwashawishi
wafadhili kuvutiwa na miradi husika.
“Katika kukabiliana na ushindani hatuna budi kujikita katika weledi na kuandika maandiko yenye kuweza kuvutia wafadhili ili waweze kuja kuwekeza nchini kwetu, ili tuweze kutimiza ndoto zetu za kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025” alisema Bibi Mwanri.
Mwezi Juni mwaka 2011, Serikali
iliandaa Mpango wa Kwanza wa Maeneleo (2011/12 – 2015/16) kwa lengo
la kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambapo Mpango huu
ulihitaji takribani trilioni 40 ili kutekeleza miradi mbali mbali ya
maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano.
Kwa mujibu wa Mpango huo, vyanzo vya
utekelezaji wake ni pamoja na Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi (PPP); uwekezaji wa kigeni; Hati Fungani kwa Waishio
Ughaibuni; Hatifungani za ndani; Hati Fungani katika Masoko ya Nje;
Mifuko ya Pensheni na hifadhi ya jamii; na makubaliano ya ushirikiano
wa kiuchumi wa nchi zinazoendelea.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni