Mahakama ya Pretoria imeambiwa kuwa
kiongozi wa genge la gerezani ametishia kuondoa uhai wa mwanariadha
mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, iwapo atapatiwa upendeleo
akiwa jela.
Kiongozi huyo wa genge Khalil
Subjee, ambaye anajulikana kama jenerali, amesema ataagiza kuuwawa
mwanariadha huyo, iwapo umaarufu wake utamfanya asipate wakati mgumu
gerezani.
Wakili anayemtetea mwanariadha huyo
Barry Roux amenukuu habari iliyoandikwa kwenye gazeti moja na kusema
kuwa maisha ya Pistorius yatakuwa hatarini iwapo atafungwa jela kwa
kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Roux amesema Subjee, anayeongoza
magenge 26 ya uhalifu na anayehofiwa mno amedai yeye ni kiongozi wa
gereza na kutoa vitisho dhidi ya Pistorius katika mahojiano
aliyoyafanya kwa njia ya simu akiwa gerezani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni