Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
amejitapa kuwa Chelsea itashinda taji katika ligi ya nchi yoyote
kutokana na kiwango ilichonacho timu hiyo hivi sasa.
Mourinho ambaye kwa sasa timu yake
inaongoza Ligi Kuu ya Uingereza kwa tofauti ya pointi tano ametoa
majigambo hayo baada ya jana kuifunga Crystal Palace mabao 2-1 katika
mchezo uliopigwa kwenye dimba la Selhurst Park.
Hata hivyo Kocha wa Crystal Palace,
Neil Warnock amesema refa aliyechezesha mchezo huo Craig Pawson
alishawishika na vitendo vya wachezaji wa Chelsea na kupelekea kumpa
kadi nyekundu mchezaji wake Damien Delaney.
Oscar akifurahia goli
Nayo timu ya Manchester City
iliitundika Tottenham mabao 4-1 huku Muargentina Sergio Aguero akipachika mabao yote manne.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni