Mwanazuoni maarufu Afrika Mashariki
na duniani kwa ujumla Profesa Ali Mazrui amezikwa leo kwenye makaburi
ya Mazrui mkabla na Fort Jesus, huko Mombasa katika eneo la Old Town.
Mapema leo usalama uliimarishwa
Mombasa Kenya wakati ambapo mamia ya waombolezaji walipouaga mwili wa
mwanazuoni huyo.
Mwili wa Profesa huyo aliyefariki
dunia Oktoba 13 nchini Marekani uliwasili leo majira ya saa tisa
usiku, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi, na kupelekwa
kwenye nyumba yake iliyopo Old Town karibu na Fort Jesus.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni