Mshambuliaji Lionel Messi amebakisha
kupachika wavuni mabao mawili tu, ili kuweka rekodi ya mchezaji
aliyefunga magoli mengi katika ligi kuu ya Hispania maarufu kama La
Liga, baada ya kufunga bao dhidi ya Eibar.
Katika mchezo huo ambao nusu ya
kwanza iliisha bila ya kupatikana bao lolote, Messi alimpatia pande
Xavi na kupachika bao wavuni lililomshinda kipa Xabi, na baadae
Neymar alipachika bao kabla ya Messi kukamilisha bao la tatu na
kufanya matokeo kuwa 3-0.
Matokeo mengine ya jana katika ligi
hiyo yalikuwa Levante 0 - 5 Real Madrid,
Athletico Bilbao 1 -1 Celta de Vigo
na Córdoba 1 - 2 Málaga.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni