Kundi la Kanisa Katoliki linalotetea
haki za mashoga, limekerwa na uamuzi wa maaskofu kupinga wito wa
kanisa hilo kuwakubali mashoga, wito ambao unaungwa mkono na Papa
Francis.
Rasimu ya ripoti hiyo ambayo pia
ilikuwa inalitaka kanisa kuwavumilia wanandoa waliotengana na kuoa
tena, ilishindwa kupata theluthi mbili ya maaskofu wanayoiunga mkono
katika Sinodi huko Roma.
Ripoti rasmi ya mwisho imeeleza kuwa
suala pekee litakalofanywa ni kwa wanaopinga mashoga kujiepusha na
kuwanyanyapaa mashoga.
Papa Francis ameagiza ripoti hiyo
yote, ikiwemo mapendekezo yaliyokataliwa kuchapishwa. Sinodi ya
Maskofu wa Kanisa Katoliki watakutana tena mwakani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni