.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 26 Oktoba 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) majukumu wanayotekeleza katika kuhakikisha wanakabiliana na tatizo la Mgongo wazi na Vichwa vikubwa ikiwamo kutoa elimu bora kwa madaktari wanaosomea somo hilo, kwenda mikoani kutoa tiba kwa watoto wenye matatizo hayo,wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na na Mgongo wazi duniani leo Jijini Dar es salaam. Kushoto ni mwenyekiti wa chama cha wazazi wenye watoto wa kichwa kikubwa na mgongo wazi(ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub.
Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub akitoa rai kwa watanzania wanaoguswa na tatizo hili kujitokeza na kusaidia chama hicho ikiwa ni njia ya kuwasaidia watoto wenye tatizo hilo ili kuokoa maisha yao kwa mpaka sasa Chama kina mfadhili mmoja.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma.
Baadhi ya wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi waliojitokeza katika sherehe hizo za Maadhimisho ya ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na na Mgongo wazi duniani yaliyofanyika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi waliojitokeza katika sherehe hizo za Maadhimisho ya ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na na Mgongo wazi duniani yaliyofanyika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Bi. Germana Gasper akitoa maaelezo kwa wananchi waliojitokeza katika banda wakati wa sherehe na kuwaasa wazazi hasa wakike waliokatika umri wa kubeba mimba kutumia vyakula vyenye vitamin ya Foliki kama maembe, Mchicha, Mihogo,machungwa, maharage, mahindi,mayai, ndizi, parachichi, papai, maini na kabichi, ili kukabiliana na tatizo la Kichwa kikubwa na Mgongo wazi kwa watoto wanaozaliwa.
Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akiteta jambo na moja ya mtoto mwenye tatizo la kichwa kikubwa anayepata huduma Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI).
Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma(Kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub(mwenye T-shirt nyeupe) na Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani leo Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dkt. Othmani Kiloloma akimlisha keki Moja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa wakikata keki katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani leo Jijini Dar es salaam.
Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akimlisha keki mmoja ya mtoto mwenye tatizo la Kichwa Kikubwa katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi duniani leo Jijini Dar es salaam
Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Bw. Abdulhakim Bayakub.
Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akiwapa msaada kinamama wenye watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi.
Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akiwapa msaada kinamama wenye watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi.
Mlezi wa Chama cha Wazazi wenye Watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBHAT) Mama Dorcas Membe akiwapa msaada kinamama wenye watoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi.

                                                                      PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni