.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 25 Oktoba 2014

MH MWANDOSYA AMUWAKILISHA RAIS KIKWETE KWENYE SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA ZAMBIA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara maalum.Mhe. Mark Mwandosya akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kenya Mhe William Ruto wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Mhe. Mwandosya alimuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe hizo. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara maalum,Mhe. Mark Mwandosya na mkewe Lucy Mwandosya wakisalimiana na Rais wa kwanza wa Zambia Mzee Kenneth Kaunda wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Mhe. Mwandosya alimuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe hizo ambazo zimefanyika Mjini Lusaka jana.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara maalum,Mhe. Mark Mwandosya (wa tatu kulia ) pamoja na Mkewe Lucy Mwandosya wakishiriki kuimba Wimbo wa Taifa wa Zambia wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana. Wengine kutoka kulia ni Kaimu Rais wa Zambia Mhe Edgar Lungu ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi, na wa pili kulia ni Makamu wa Rais wa Nigeria Monance Namadi Sambo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni