Mfalme wa Pop marehemu Michael
Jackson ameendelea kuingiza kipato kikubwa licha ya kufariki dunia
miaka mitano iliyopita.
Michael Jackson kwa mara nyingine
tena amempita marehemu Elvis Presley na kuwa supastaa aliyekufa
anayeongoza kwa kuingiza kipato katika mwaka 2014.
Mfalme huyo wa Pop ameendelea
kuingiza fedha akiwa kaburini, hata kuliko mastaa waliohai, ambapo
imeelezwa ameingiza kiasi cha dola milioni 140.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes,
marehemu Michael Jackson ameingiza fedha mara tatu zaidi ya marehemu
Elvis Presley, ambaye aliingiza dola milioni 55, katika kipindi kama
hicho cha miezi 12.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni