Afisa mmoja wa Kikurdi amesema
wapiganaji wa Kundi la Dola ya Kiislam (IS) wanajiondoa katika maeneo
ya Mji wa Kobane nchini Syria.
Kiongozi huyo Idriss Nassan
ameiambia BBC, IS wamepoteza asilimia 20 ya maeneo ya mji huo
waliyokuwa wanayashikilia katika siku za hivi karibuni.
Maafisa wa Ulinzi wa Marekani
wamesema mamia ya wapiganaji wameuwawa katika maeneo ya Mji wa
Kobane, kufuatia mashambulizi ya anga yanayoongozwa na Marekani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni