Muuguzi aliyepata maambukizi ya Ebola
Rais Barack Obama ameondoa uwezekano
wa kuwepo wa mlipuko wa Ebola nchini Marekani, kwa kusema hatari ya
Wamerikani kupata maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo ipo chini mno.
Rais Obama ametoa kauli hiyo baada
ya muuguzi wa pili Marekani kuambukizwa Ebola baada ya kumtibu raia
wa Liberia ambaye aliyefariki kwa ugonjwa wa Ebola huko Dallas.
Wakati huo huo, Mkuu wa Umoja wa
Mataifa ameonya kuwa nchi za Afrika Magharibi, zinakabiliwa na
uwezekano wa mgogoro wa chakula kutokana na mlipuko wa Ebola.
Ugonjwa huo umeuwa watu 4,500 hadi
sasa wengi wao kutokea nchi za Liberia, Guinea pamoja na Sierra Leon.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni