Mvua kubwa iliyonyesha kwa saa nane
katika kijiji cha Nyamikoma kata ya Kabita wilayani Busega,
imesababisha watu 215 kukosa makazi huku nyumba 46 zikianguka.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake
waliothirika na mvua hiyo, Paul Mchele, amesema familia yake ya watu
11 kwa sasa haina pa kuishi baada ya mvua hiyo iliyoanza saa 10.45
alfajiri na kukatika saa 6 mchana kusomba kila kitu.
Mtendaji wa kijiji hicho, Juma
Msema, amesema mvua hiyo imesababisha majanga makubwa kutokana na
mvua hiyo kusababisha mafuriko lakini anashukuru kwa kutoripotiwa
kifo cha aina yoyote ingawa wananchi wamepoteza mali zao.
Mkuu wa wilaya hiyo, Paul
Mzindakaya, ameiagiza kamati ya maafa kufanya tathimini ya haraka ili
kuwasaidia waathjirika hao.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni