Watu wawili wa familia moja
wamefariki dunia baada ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu
katika kijiji cha Miranda tarafa ya Nshamba wilayani Muleba, huku
watoto wengine wanne wakiwa hospitalini wakipatiwa matibabu.
Kamanda wa polisi mkoani Kagera,
Henry Mwaibambe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja
waliopoteza maisha kwa madai ya kula ugali wa muhogo ni Oliva Wilson
miaka 42 na Nemilius Wilson miaka mitano.
Amesema watoto wengine wanne wa mama
huyo Avira Wilson miaka 10, Frolida na Frola Wilson mapacha wenye
miaka saba na Scarion Wilson miaka miwili, wamelazwa katika hospitali
ya wilaya ya Rubya.
Kamanda Mwaibambe amesema unga
wanaosadikiwa kuutumiwa kwa ugali watu hao, umekusanywa na kupelekwa
kwa mkemia mkuu wa serikali kwa ajili ya vipimo ili kubaini kama
ulikuwa na sumu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni