.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 22 Oktoba 2014

WASANII WA MUZIKI - MWANA FA, BARNABA, CPWAA, FID Q NA VENESSA MDEE WAJIUNGA NA BARCLAYS KUCHANGIA TAMASHA LA MATEMBEZI YA HISANI YA STEP AHEAD


  Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Benki ya Barclays leo watangaza rasmi wasanii wa Bongo Flava watakao tumbuiza watanzania kwenye tamasha la Step Ahead tarehe 25 Oktoba kwenye uwanja wa Leaders. Kusudi la tamasha hili ni kuchangisha fedha zitakazotumiwa kuwasaidia afya ya  Mama na watoto wachanga.

Akiongea kwa niaba ya Barclays , Mr. Musa Kitoi, Mkuu wa kitengo cha Bidhaa, Uchuuzaji na Mikakati alisema ; “ Barclays imeandaa matembezi/mbio za hisani kuchangia afya ya Mama mzazi na mtoto nchini Tanzania. Benki ya barclays imeteua afya ya uzazi wa mama na mtoto kama jukumu lake kuu la kihisani.  

Tanzania ni moja ya nchi zilizo nyuma kutekeleza mikakati miwili ya malengo ya milenia inayolenga uboreshaji wa afya ya mama mzazi na mtoto. Takwimu zinaonyesha kuwa Kiwango cha vifo wakati wa uzazi ni 454 katika kila vizazi 100,000.

Tunaamini tunaweza kuchangia na kuleta mabadiliko chanya katika kuwawezesha na kuimarisha utendaji wa wauguzi na wakunga wa jadi. Sisi kama benki tuko katika nafasi nzuri ya kukusanya rasilimali kwa ajili ya kusaidia swala hili muhimu. Ni imani yetu kwamba taifa bora linawezekana iwapo wakina mama na watoto watakua na afya bora.Benki ya Barclays inashirikiana na CCBRT na AMREF kukabiliana na jambo hili. Fedha zote na matumizi yatadhibitiwa na kamati ya jamii ya uwekezaji, chini ya Benki ya Barclays. 


Mwaka wa 2011 na 2013 Barclays ilichannga zaido ya milioni 337. Mwaka huu inatarajia kuchanga Milioni 200, hela hii itatumika kwa mafunzo kwa wakunga wa jadi na kuimarisha uwezo wao wa kusaidia akinamama kujifungua salama. Matibabu maalumu kwa watoto wanaozaliwa na kasoro zinazorekebishika kimaumbile na kununua vifaa vya afya vinavyotumika katika kitengo cha uzalishaji.

Barclays inawashukuru wanamuziki Mwana FA, FID Q, Barnaba, Vanessa Mdee na CPWAA  kuwapongeza kwa kuwa kwenye mstari wa mbele kuchangia na kuleta mabadiliko chanya katika maendeleo ya kijamii.

-End-
 
Kwa Maelezo zaidi:
Neema-Singo Rose
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano
Barclays Bank Tanzania
+255 22 2282018

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni