.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 20 Oktoba 2014

UBINGWA WA SAFARI POOL AFRIKA 2014 WAENDA AFRIKA KUSINI


Mabingwa wa Safari Pool Afrika 2014 kutoka Afrika Kusini, timu ya Taifa ya Pool ya Nchi hiyo wakishangilia na kitita cha Dolla 5000$ sawa na pesa taslimu za Kitanzania Shilingi 8,500,000/= pamoja na medali za dhahabu baada ya kutwaa ubingwa huo uliojulikana kwa “Safari All Africa Pool Championship 2014” uliomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaaam.
Rais wa Chama cha Pool Africa(AAPA), Saths Reddy(kulia) akimkabidhi Meneja wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini ya mchezo wa Pool, kitita cha Dolla 5000 sawa na pesa taslimu za kitanzania 8,500,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Pool Africa(AAPA), Saths Reddy(kulia) akimkabidhi Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo wa Pool kitita cha Dolla 2000 sawa na pesa taslimu za kitanzania 3,400,000/= mara baada ya kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Taifa wa mchezo wa Safari Pool Tanzania, wakishangila wakiwa na kitita cha Dolla 2000$ sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 3,400,000/= pamoja na medali za Silva mara baada ya kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles), Ishmael Mthethwa kutoka Afrika Kusini akionyesha kitita cha Dolla 2,000 sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 3,400,000/= pamoja na medali ya Dhahabu mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni