Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,Kanali
mstaafu Issa Machibya akiongea na waandishi wa habari(ambao hawapo
pichani)ofisini kwake juu ya kusitisha kwa zoezi la uopoaji wa miili
ya ajali ya mitumbwi iliyotokea hivi karibuni katika kijiji cha
kalalangabo ziwa Tanganyika.
Na Editha Karlo wa blog ya
jamii,Kigoma
Serekali ya Mkoa wa Kigoma
imesitisha zoezi la uopoaji wa miili ya ajali ya mitumbwi miwili ya
maharusi iliyotokea tokea hivi karibuni katika Ziwa Tanganyika kwenye
kijiji cha Kalalangabo kilichopo mwambao mwa ziwa Tanganyika .
Akiongea na waandishi wa habari
ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya
alisema kuwa vikosi mbalimbali vya ukoaji kwa kushirikiana jeshi la
wananchi(JWTZ)wakishirikiana na wananchi wamefanya kazi kubwa sana ya
kuopoa miili kwa kipindi cha siku tatu mfululizo.
Amesema jumla ya miili kumi ili
patikana katika zoezi hilo la ukoaji lakini hivi sasa wameachia
uongozi wa kijiji cha serekali ya kalalangabo kuendelea kutoa taarifa
kama kuna miili mingine itakayoibuka kutokana na kuhofiwa kuwa bado
miili mingi ipo majini
Mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi
kuacha tabia ya kutumia vyombo visivyo rasmi katika usafiri na
ambavyo havijasajiliwa na mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini
(SUMATRA)pia aliwataka wavuvi na wale wenye vyombo majini waache
tabia ya kusafirisha abiria kwa kutumia mitumbwi ya kuvulia dagaa ili
kuepuka ajali.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni