Mabinti wa Rais Barack
Obama, Sasha na Malia wametuhumiwa kuonyesha kutokuwa na heshima na
hawana viwango na afisa mmoja wa chama cha Republican baada ya
kuonekana katika hafla ya sherehe za Thanksgiving wakiwa wamevalia
vimini.
Afisa huyo Elizabeth
Lauten, ambaye ni mkurugenzi wa mawasiliano wa mjumbe wa Baraza la
Congress Stephen Fincher, aliandika hayo kupitia ukurasa wake wa
Facebook, na kisha kufuta, baada ya kushambuliwa mno kwa kutoa
maneono yenye kuumiza, ambapo pia ameomba msamaha.
Lauten aliwatuhumu pia
mabinti hao wa rais Obama, walionekana wakiwa wameboreka wakati
wakiwa wamesimama pamoja na baba yao, katika kitendo cha utumaduni wa
Ikulu kuwaachia huru batamzinga wawili ili kuwaepusha kutumika kama
mlo wa jioni wakati wa sherehe za Thanksgiving.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni