Bondia Tyson Fury
ameshinda mataji mawili ya mkanda wa uzito wa juu wa Uingereza na
Ulaya, katika raundi ya 10 kwenye pambano lake na bondia aliyesalimu
amri Dereck Chisora kwenye ukumbi wa ExCel arena, Jijini London.
Bondia huyo wa
Manchester, Fury, ambaye alimzidi pinti Chisora mwaka 2011,
alibadili staili ya kupigana katika raundi ya pili na kumudu kutawala
kila dakika ya mchezo huo katika kila raundi.
Bondia Chisora ambaye
makazi yake yapo London, katika mchezo huo alionekana kabisa
kushindwa kuonyesha makali yake, na pia kushindwa kudhibiti makombora
ya mpinzani wake Tyson Fury.
Kwa ushindi huo Fury
anajipanga kupigana na bingwa anayeshikilia mikanda ya uzito wa juu
ya WBA, IBF na WBO mrusi Wladimir Klitschko.
Tyson Fury akimpa uppercut bondia Dereck Chisora
Bondia Dereck Chisora hoi akipatiwa tiba katika jeraha alilopata
Refa wa pambano hilo akitoa ishara ya kumaliza pambano katika raundi ya kumi




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni